UGONJWA wa mawe kwenye figo siyo mgeni miongoni mwa watu hivi sasa, hasa wenye umri mkubwa. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, ukubwa wa tatizo hili umeongezeka, kwani hata vijana wanapatwa na tatizo hili ambalo kitalaamu linajulikana kama ‘Gallstones’. 

Mawe ya kwenye figo siyo mawe halisi, bali huwa ni vitu vinavyojitengeneza kwenye figo taratibu na baada ya muda mrefu hugeuka umbo na kuwa mfano wa vijiwe vidogo na wakati mwingine huwa vikubwa mfano wa dole gumba. Hutokana na ulaji wa vyakula usio sahihi.