Pages

Sunday, January 20, 2013

Njia salama isiyo na gharama kwa kutunza ngozi yako

  1. Epuka uvutaji wa aina yoyote, mfano sigara bangi  madawa ya kulenya, petrol, na mambo mengine kama hayo. Kuvuta kuna madhara mengi kiafya kwenye mwili pamoja na magonjwa ya moyo na cancer ya mapafu.Hata hivyo kitu watu wengi hawajui ni kwamba nicotine ambayo iko kwenye sigara unapovuta inaweza kubadilisha rangi ya ngozi na wakati mwingine kuota chunusi.Ili uweze kuwa na ngozi nzuri ni lazima uache kabisa kuvuta.
  2. Vitamin A na E , wakati unaendelea kuwa mtu mzima ngozi inaanza kupoteza uzuri wake, kwa sababu cell, collagen na elastin zinaanza kupungua nguvu matokeo yake ni wrinkles na matatizo mengine ya ngozi. Matumizi ya vitamin A na E supplement zenye ( collagen na elastin) vyaweza kuzuia ngozi kuharibika. Vitamin A na E pamoja na madini ya asili vimethibitisha kuongeza uwezo wa cell za ngozi, hivyo inaongeza ubora na muonekano wa ngozi.
  3. Epuka kutumia mafuta ya mgando kwenye ngozi, mafuta yanaziba pols na kusababisha chunusi, chunusi zaweza kusababisha makovu usoni , na hivyo kupoteza kabisa muonekano mzuri wa ngozi yako. Wakati unapotumia product za ngozi tumia mabazo hazina mafuta pia ambazo  hazina harufu ( fragarance).
  4. Punguza matumizi ya sukari, haswa soda na chai, matumizi ya vyakula vya kukaanga, kama chips na vinginevyo. Nyama nyekundu na maziwa ( diary product) unashauriwa kuacha kabisa kwa sababu mara nyingi husababisha allergy. Kunywa maji mengi, kula matunda na mboga za kutosha, lala mapema ikiwezekana kabla ya saa tatu na nusu. Usioshe uso na sabuni jitahidi kutumia cleaser.
Angalizo
Jitahidi kupata ushauri wa Doctor mara zote unapotaka kutumia vipodozi vipya au kupadili vipodozi.

0 comments:

Post a Comment