Saratani au kansa ni aina za ugonjwa unaoanzishwa na seli za mwili zinazoanza kujigawa yaani kukua bila utaratibu na bila mwisho. Ukuaji huu unaleta uvimbe mwilini unaozidi kuwa kubwa hadi inabana viungo vya mwili kama neva, mishipa ya damu, ubongo, mapafu, maini, utumbo na kadhalika na kuzuia visifanye kazi. Pamoja na hayo kansa / saratani huwa na tabia za kujisambaza mwilini mahali pengi baada ya muda fulani na kusababisha kutokea kwa vimbe nyingi mwilini vinavyoendelea kukua hovyo. Kama uvimbe hauna uwezo wa kusambaa seli zake mwilini na kusababisha vimbe mpya si saratani.
Kansa inaweza kutokea kwa mtu yeyote lakini hutokea zaidi kwa watu wenye umri mkubwa na watu anaoathiriwa na kemikali mbalimbali. Katika nchi zilizoendelea ambako wanachi hufikia umri mkubwa saratani iko kati ya sababu kuu za kifo.
0 comments:
Post a Comment