Vitunguu vikubwa 6,
Pilipili hoho 2,
Nyanya 4 kubwa,
Cabbage 1 kubwa,
Leeks
kubwa 4,
Cube 2 za Knorr au Roiko (kwa ladha na si lazima). Hii inaweza kutosha
kwa nusu siku mpaka siku nzima kutegemea uwezo wako wa kuila. Boresha ladha kwa kuongeza chumvi, pilipili kawaida au manga, hot sauce au
malimao/ndimu.
Namna ya kutengeneza:
Katakata mboga viwe vipande vidogodogo. Weka maji yajae kufunika mboga. Chemsha
haraka kwa muda wa dakika kumi halafu punguza moto zitokote taratibu mpaka
zilainike kabisa. Baada ya hapo saga kwenye blender au utakavyoweza ili upate supu yenye
rojorojo.
Kula hii supu kwa kadiri uwezavyo kwa kuwa haita ongeza calories kwenye mwili.
Jinsi utakavyo kula hii supu ndivyo utakavyo pungua uzito. Ni vema kuweka supu kwenye thermos asubuhi kama hautakuwepo nyumbani ili
uendelee kula mahali popote utakapo kuwa.
UKILA HII SUPU PEKE YAKE KWA MUDA MREFU SANA UNAWEZA KUPATA UTAPIAMLO (MALNUTRITION).
SIKU YA KWANZA
· Kula matunda aina yeyote isipokuwa ndizi.
· Matikiti maji yana calories chache kuliko matunda mengine kwa hiyo ni bora kula hayo.
· Siku hii kula supu peke yake na matunda.
· Kunywa chai isiyo na sukari pamoja na maji.

SIKU YA PILI
· Kula mboga aina yeyote ile.
· Kula mpaka ushibe mboga ambazo ni fresh kama vile saladi au mboga za majani zilizosindikwa kwenye kopo.
· Usile maharage yaliokaushwa, njegere au mahindi makavu.
· Kula hizo mboga pamoja na supu.
· Kwa chakula cha jioni siku hii unaweza kula kiazi kimoja kikubwa kilicho okwa na unaweza kupakaa siagi.
· Usile matunda ya aina yeyote nyingine.
SIKU YA TATU
· Kula supu, matunda na mboga za majani aina yeyote.
· Usile kiazi kilicho okwa.
Kama utakuwa umekula kama ilivyo onyeshwa hapo juu, na huja danganya, basi utakuwa umepoteza uzito wa mwili kwa wastani wa kilo 2 mpaka 3 baada ya siku hii ya tatu.

SIKU YA NNE
·Kula ndizi mbivu na maziwa yaliyopunguzwa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula ndizi mbivu tatu, maziwa glasi nyingi uwezavyo pamoja na supu.
SIKU YA TANO
· Kula nyama ya Ng’ombe na nyanya fresh.
· Kula nyama kiasi cha robo mpaka nusu kilo pamoja na nyanya fresh kadiri uwezavyo.
· Jaribu kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji ili kupunguza uric acid kwenye mwili.
· Kula supu angalau mara moja siku hii.
SIKU YA SITA
· Kula kiasi chochote cha nyama ya Ng’ombe na mboga za majani. Ni bora kula saladi kwa wingi pamoja na nyama, lakini usile kabisa Viazi siku hii.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.
· Kula kiasi chochote cha nyama ya Ng’ombe na mboga za majani. Ni bora kula saladi kwa wingi pamoja na nyama, lakini usile kabisa Viazi siku hii.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.
SIKU YA SABA
· Kula wali, juice isiyo na sukari na mboga za majani. Kula kadiri utakavyoweza.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.
Inategemewa kuwa baada ya siku ya saba utakuwa umepoteza kati ya kilo 4.5 mpaka 7.7 ya uzito wa mwili.
Kama umepoteza zaidi ya kilo 6.8 simama kwanza kwa siku mbili kabla hujaendelea na huu utaratibu wa mlo tena.
Utakapo anza tena, anzia siku ya kwanza na kuendelea mpaka siku ya saba tena.
Kwa kuwa miili ya binaadamu inatofautiana, diet hii italeta mabadiliko tofauti tofauti kutegemea mwili unavyo ipokea. Kawaida baada ya siku tatu mwili wako utajisikia nguvu zaidi kama hujadanganya.
VITU VISIVYO RUHUSIWA KABISA WAKATI WA DIET HII.
· Hairuhusiwi kutumia Mkate, Pombe aina yeyote, vinywaji vyenye gesi kama vile soda na vyakula vilivyo kaangwa na mafuta.
· Hairuhusiwi kutumia Mkate, Pombe aina yeyote, vinywaji vyenye gesi kama vile soda na vyakula vilivyo kaangwa na mafuta.
· Tumia maji, chai isiyo na sukari, kahawa isiyo na maziwa wala sukari, juice za matunda zisizo na sukari na maziwa yalio ondolewa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula Kuku aliochemshwa au kuokwa badala ya Nyama, lakini uondoe ngozi yake. Unaweza vilevile kutumia Samaki aliyechemshwa katika siku moja inayohitaji Nyama badala ya Nyama lakini sio zaidi ya siku moja.
· Supu hii inaweza kutumika saa yeyote unapo hisi njaa. Kunywa uwezavyo. Kumbuka jinsi unavyo inywa kwa wingi ndivyo unavyo punguza uzito.
Supu hii haingiliani na dawa zozote utakazo andikiwa.
Endelea na utaratibu huu mpaka utakaporidhika kuona mabadiliko katika mtazamo na mwili wako.
ANGALIZO
Hii soup inapunguza mwili kwa haraka sana ila ukishapungua inabidi uangalie mlo wako inabidi upunguze vyakula vya mafuta mawali maugali badala yake ule mboga nyingi kuliko chakula, sio baada ya wiki unaanza kufakamia misosi mfululizo utanenepa zaidi ya mwanzo.
0 comments:
Post a Comment